Jumamosi , 13th Jun , 2015

Rapa Joh Makini, ametoa mtazamo wake kuhusiana na uzuri na ubora wa muziki wa zamani ukilinganishwa na ule unaofanyika sasa

Shetta, Joh Makini & Nah Reel

Rapa Joh Makini, ametoa mtazamo wake kuhusiana na uzuri na ubora wa muziki wa zamani ukilinganishwa na ule unaofanyika sasa na kusema kuwa mtazamo huo unachangiwa na mabadiliko ya sanaa hiyo kulingana na kizazi husika, swala la uzuri na ubaya wa muziki wenyewe likiwa linahusika pande zote mbili.

Star huyo ambaye anafanya vizuri katika chati za muziki wa kizazi kipya akiwakilisha miondoko ya Hip Hop, amekazia kuwa kila muziki unabeba uzuri wake kulingana na kizazi husika.

Joh Makini amezungumzia haya kuonesha msimamo wake kuhusiana na mtazamo kuwa muziki na wasanii waliokuwa wanafanya sanaa hiyo zamani ndio wanasanaa na muziki wao ndo wa kweli zaidi kuliko ule ambao unafanyika sasa.