Jumatano , 2nd Oct , 2019

Msanii maarufu nchini Uganda ambaye kwa sasa ameanza kujihusisha na masuala ya siasa Jose Chameleone, ameuweka hadharani ujumbe wa mtu anayemtishia maisha, endapo atashindwa kumtumia kiasi cha pesa alichomuomba.

Jose Chameleone

Kupitia ujumbe wake aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook, Chameleon amesema baada ya kufuatilia usajili wa namba hiyo alikutana na jina la Jenifer Maniraduha, tofauti na awali ambavyo mtu huyo alijitambulisha kwa jina la Generali.

"Tahadhari, nimekuwa nikipokea vitisho kutoka kwenye namba hii (akiitaja), mtu ambaye amejitambulisha kwa jina la Generali, mara ya kwanza alinitumia ujumbe  Septemba 10 saa 12 jioni na alitaka nimtumie shilingi 5,000,000 la sivyo ataniua ila nilipuuzia, leo tena amenitumia ujumbe wa kutaka 8,000,000 kama nisipotuma ataniangamiza", ameandika Chameleon.

Chameleone ameongeza kuwa hadi sasa tayari amevitaarifu vyombo vya usalama na wamemuahidi kufanya uchunguzi juu ya suala hilo.