Jumanne , 29th Jun , 2021

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Uganda aliyetamba na ngoma kama Katupakase na Jamila, Jose Chameleone (42) ameweka wazi kuwa atastaafu kufanya muziki pindi atakapofikisha umri wa miaka 50. 

Picha ya msanii Jose Chameleone

Chameleone ni miongo mwa wasanii waliofanya makubwa kwenye soko la muziki katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ambapo amesema ifikapo mwaka 2029 hatoweza tena kuendelea na shughuli za muziki.

“I’m 42 years old, I only have 8 years to make 50, at 50 I will be tired so I will have to slow down, I don’t want to jump on stages for my entire life” – amesema Jose Chameleone