Alhamisi , 12th Dec , 2019

EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na mkali wa RnB Bongo, Juma Jux, ambaye amefunguka kuhusu tabia ya kupenda wanawake ambao wana maumbo membamba ya 'umodo'.

Msanii wa RnB Juma Jux.

Ukiangalia wapenzi wa zamani wa msanii huyo kama video vixen Jack Cliff, msanii Vanessa Mdee na mpenzi wake wa sasa aitwaye Nnayika, wote utagundua wanamaumbo membamba, hali inayopelekea watu kuhisi Jux anapenda wanawake wenye sifa hiyo.

Kwa upande wa Juma Jux ameeleza kuwa "Inatokeaga kupenda wa style hiyo ila mimi kuna vitu vyangu ambavyo naviangalia kwa msichana na hivyo vitu vingine vinakuja baadaye, inawezekana ikawa kwa watu ambao wananifuatilia kuwa wameona na wamejua hivyo".

Aidha Jux ameendelea kusema "Lakini  huwa sisema kwamba mwanamke fulani akiwa hivi ndiyo nitampenda, hivyo vinakuwaga vitu vyangu vya mwisho baada ya kuangalia vitu vingine, kwanza mtu ninayemtaka inabidi ajielewe sana, awe msafi, na anipende kama nilivyo kisha ndiyo vinakuja hivyo" ameongeza.