Jumatano , 29th Jun , 2022

Kinyozi wa wasanii J4 Barbershop amesema Jux sio mtu ambaye anahesabu fedha wakati wa malipo akimaliza kumnyoa bali anazama mfukoni na kutoa pesa zozote.

Picha ya Jux akiwa ananyolewa nyumbani kwake

Akipiga story na Planet Bongo ya East Africa Radio J4 amesema

"Kunyoa kawaida ni Tsh 10000, ila kwa style kama ya Jux ni 40,000 lakini yeye akiingia mfukoni huwa ahesabu anatoa burungutu unakuta laki na hamsini au laki mbili"

"Wasanii wote ni wacheshi lakini Barnaba Classic kazidi akija tu huwa ana-smile muda wote na mtu wa story, wasanii wengine inategemea na moods zao".