Alhamisi , 3rd Oct , 2019

Wikiendi iliyopita kulifanyika maonyesho ya pili ya mavazi "Tanzania Fashion Festival" ambayo hukutanisha watanamindo na wabunifu wa mavazi kuonyesha bidhaa zao, ambapo safari hii lilihudhuriwa na mastaa kama Jux na Jacqueline Wolper.

Juma Jux akiperforme kwenye tamasha hilo

Licha ya kufanyika tamasha hilo pia walikuwa wanasheherekea mavazi ya majira ya joto , kukutanisha wapenzi wa muziki wa Jazz, vyakula , vinywaji pamoja na mtoko wa kifamilia ambao hukutanisha watu mbalimbali.

Muandaji wa onyesho hilo la ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha NIRVANA cha East Africa Television, Deogratius Kithama amesema, nia ya tamasha hilo ni kuleta pamoja wapenzi wa mitindo na wanaopenda 'lifestyle' kwa ujumla na kutoa wabunifu wa mavazi kutokea Tanzania.

"Tumekuwa na bahati sana kwa sababu mwaka huu tumeona mabadiliko na maendeleo makubwa katika tamasha hili ukianzia maandalizi, mahudhurio ya watu na  hali hii inaonyesha kiasi gani tasnia ya mitindo inakuwa kila siku" ameeleza.

Akizungumzia uwepo wa ushindani wa mavazi waliyoonyesha kati ya Juma Jux na Jacqueline Wolper kwenye tamasha hilo Deogratius Kithama amesema,

"Wote wana "style" mbili tofauti ila nilinivutiwa na Jux alivyobadilisha bidhaa zake ambapo ameleta usasa mpya kwa kuongeza vitu mbalimbali kwa dizaini tofauti. Aidha kwa upande wa Wolper  wote tunamfahamu ni Mama wa maigizo alienda hadi Dubai kufanya manunuzi ili kuleta "material" ya kuonyesha katika tamasha hili"  ameongeza.

Pia amemaliza kwa kusema wote walitumia nguvu , gharama , muda na ubunifu katika onyesho hilo la mavazi "Tanzania Fashion Festival", ili kuhakikisha linakuwa la tofauti na matamasha mengine kwani ndio ilikuwa shauku yao.