Jumatatu , 20th Dec , 2021

Lulu Diva anasema mama yake alikuwa anampa sapoti kubwa kwenye mambo anayoyafanya pia alikuwa anatamani kufanya vitu vingi lakini hali ya afya na umri ulikuwa haumruhusu.

Picha ya Lulu Diva akiwa na mama yake mzazi

Akimzungumzia mama yake enzi za uhai wake Lulu Diva anasema ni mama ambaye alikuwa anamsihi asikate tamaa, afanye bidii na kuendelea kufanya kazi.

Pia amesema mama yake alikuwa anamwambia asifananishe kifo na usingizi kwa sababu yeye ni mtoto wa kimaskini hivyo apambane asijifananishe na matajiri.

Taarifa za kifo cha mama Lulu Diva zimetoka siku ya jana na msiba upo Kunduchi Dar es Salaam karibu na kota za jeshi.

Zaidi mtazame hapa akimzungumzia mama yake.