Alhamisi , 13th Apr , 2017

Rapa Kala Jeremiah amedai alishtushwa na kauli ya msanii mwenzake Dayna Ntyange baada ya kudai kutomfahamu mbele ya Tv lakini alikuja kupuuzia baada ya kugundua alisema ki masihara japo hajawai kumuuliza.

Akiongea na eNewz ya EATV Kala Jeremiah amesema awali watu walipomwambia alishtuka na hakuamini lakini baada ya kutazama marudio ya kipindi aligundua Dayna aliongea kwa utani na wala hakutegemea kama ingekuwa ni story kubwa na kusisistiza kuwa wao ni washkaji hakuna hata ugomvi unaoendelea kati yao.

"Sitaki kuamini kama Dayna hanifahamu. Sisi ni washkaji wa muda na hata alivyodai hanifahamu huwezi amini sijawahi kumpigia simu nimuulize maana tunakutana na tunapiga story kama kawa. Hicho siyo kitu kikubwa sana kwangu cha ku-mind kwa nini anikane, kwa sababu kwanza kila mtu anajua ushkaji wetu uliopo kati yangu mimi na Dayna na ukizingatia mimi ni mmoja kati ya marafiki zake wanaoimba hip hop" Amesema Kala Jeremiah.

Wasilikilize wote, Kala na Dayna katika video hii ya eNewz.....