Jumanne , 21st Apr , 2015

Berita Khumalo, msanii wa muziki wa Zimbabwe anayefanya kazi zake za muziki huko Afrika Kusini, amezungumzia
machafuko ya Xenophobia kuwataka wazawa wa nchi hiyo kufahamu kuwa, wageni waliopo nchini mwao, wapo pia kwa faida yao.

msanii wa kike wa nchini Zimbabwe Berita Khumalo

Khumalo amesema kuwa, hali ya watu kutoangaliwa kwa usawa katika nchi hiyo ni kitu cha ajabu na hakitakiwi kuwa kinatokea katika miaka hii ya sasa, akiongeza kuwa Afrika Kusini inatakiwa kuchukua hatua kuishikilia heshima ambayo ilikuwa nayo.

Kauli ya Khumalo inaungana na nyinginezo nyingi za mastaa wa muziki kutoka Afrika, kupinga machafuko hayo ya Xenophobia.