Alhamisi , 4th Sep , 2014

Zikiwa zimebakia siku moja kabla ya kufanyika tamasha kubwa la Kilimanjaro Music Tour litakalohitimisha ziara zake kwa mwaka huu pale Leaders Club siku ya Jumamosi.

Kilimanjaro Music Tour 2014, Tanzania

Wakazi wa Dar es Salaam wameonyesha hamasa na matarajio makubwa kwa onyesho hili huku eNewz ikiambatana na timu ya East Africa Radio, imeweza kufika katika maeneo mbali mbali ikiwemo Tandika Azimio mtaa wa Maputo.

Pia eNewz imeweza kukutana na wapenzi wa burudani Mwembe Yanga walioweza kujishindia zawadi za T-Shirt, Ticketi na Fedha ya Nauli ya kufika Leaders Club jumamosi hii.