Jumanne , 22nd Jul , 2014

Msanii wa muziki Diamond Platnumz, amepatiwa cheti cha kutambua mafanikio yake, "A Certificate of Achievement" na waratibu wa Tuzo za muziki Afrika za Kora, kutokana na zoezi walilokuwa wakiliendesha mtandaoni kutambua wasanii barani Afrika.

Cheti hiki kimetolewa kutokana na Diamond kuchaguliwa na mashabiki kwa wiki 13 mfululizo akiwa kama msanii anayefanya vizuri katika kipengele cha msanii Bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki.

Diamond amepatiwa cheti hiki sambamba na wasanii wengine wakali kabisa kutoka Afrika, akiwepo Knowless Butera kutoka Afrika Mashariki, Dj Arafat, Sarkodie na Flavour kutoka Afrika Magharibi kati ya wengine.