Jumanne , 22nd Dec , 2020

Msanii wa muda mrefu hapa nchini wa Tanzania, Hussein Jumbe amefunguka kusema madhara aliyopata hadi kuvunjika mguu yametokana akiwa ndotoni ambapo ameota alikuwa anapigana na kuku.

Msanii wa muziki wa Dansi Hussein Jumbe

Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Hussen Jumbe amesema ni ngumu mtu kuamini tukio hilo ila ukweli ndiyo na mtu pekee aliyetokea kumsaidia alikuwa ni mke wake ambaye alimshutua kutoka usingizini.

"Nimevunjika mguu nikiwa ndotoni ambapo niliota napigana na kuku, mimi nilikuwa naendesha baiskeli sasa kuna mtoto alikuwa ameshika manati ambayo aliipiga baiskeli yangu, nikamfuata wakati nagombana naye ghafla akageuka kuku, mimi nikawa nampiga ili asiniparue kumbe nilikuwa napiga kitu kizito kwenye mguu nikiwa kitandani ndipo mke wangu akanisaidia" ameeleza Hussein Jumbe

Aidha Hussein Jumbe amesema alijaribu kwenda kwa watafsiri wa ndoto ambao walimwambia kuwa tukio hilo linahusisha masuala ya kishirikina.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.