Jumatano , 13th Jan , 2016

Staa wa Muziki Linex ameeleza kuwa, picha zake zinazoendelea kuzua mjadala mkubwa mtandaoni, zinazomuonesha akiwa na bibi harusi katika pozi mbalimbali, zikimuhusisha yeye kuchukua hatua ya kuoa ni kitu ambacho atakizungumzia ndani ya siku 5 zijazo.

Staa wa Muziki nchini Linex

Binafsi akishikilia msimamo kuwa ameoa na mambo mengine si lazima kutangaza sana, Linex ameiambia eNewz kuwa picha zaidi ambazo zitatoa maelezo kuhusiana na kile hasa ambacho kinaendelea zitafuata, kabla ya yeye kutoa tamko rasmi hivi karibuni.