
Tunda
Tunda amezungumza hayo leo kwenye eNewz ya EATV na kusema kuwa tangu kutajwa kwenye wahusika wa matumizi ya madawa imemfanya kubadilisha mpaka mfumo wa maisha kwa kuwa nyumbani kwa wazazi wake wamekuwa wagumu kumuelewa.
"Nimebadilisha mfumo wa maisha, naishi maisha ya low profile kwa sasa ili mambo kwanza yatulie lakini nipo. maisha ya mitandaoni nimeacha. Suala la kutajwa linaniumiza kwa sababu nyumbani haikuwa rahisi kueleweka na wazazi. Viongozi wanadai natumia mimi ndo niseme najitetea ukweli ni vigumu mno lakini naamini kwenye ukweli uongo hujitenga pembeni ipo siku ukweli utajulikana na maisha yataendelea kama kawaida. Niweke wazi situmii madawa ya kulevya". Alisema Tunda
Tunda na baadhi ya mastaa wengine wapo nje kwa dhamana baada ya kutuhumiwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya.