Jumatatu , 27th Jan , 2020

Mwanandoa mpya mjini Peter Msechu, amesema hatakuwa na masihara kwa watu watakaoleta mazoea ya kupitiliza kwa mke wake Amariss Lauren, kwa sababu anaweza kumpiga mtu risasi au kumkata shingo.

Picha ya Peter Msechu akiwa na mke wake Amariss Lauren

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, wakati wa harusi yake Peter Msechu amesema, kwa sasa hivi tayari anacheti halali cha ndoa na ambaye ataleta mazoea basi kumkata shingo ni kazi rahisi sana.

"Mtu kumpigia simu mwanamke wangu au kum-follow sio ishu kwa sababu hayo mambo yameshatokea sana ila wajue tu huyu ni mke wangu, namuheshimu na naheshimu ndoa yangu, mazoea yakizidi kuvuka mipaka hata nikimpiga mtu risasi au kumkata shingo kutakuwa hakuna kesi, maana nina cheti cha ndoa" amesema Msechu.

Ndoa ya Peter Msechu na mkewe Amariss Lauren imefanyika siku ya Januari 25,2020 na imehudhuriwa na wasanii mbalimbali tofauti wakiwemo Ben Pol, Kajala, Monalisa, Mrisho Mpoto, Esha Buheti na Alice Kella.