"Kwa waganga nakwenda sana" - Tausi

Jumatano , 14th Feb , 2018

Msanii wa  filamu nchini Tausi Mgegela amefunguka na kusema katika maisha yake kwenda kwa mganga wa kienyeji si jambo la kutisha wala geni kwani mara kadhaa ameshakwenda kwa mganga wa kienyeji kwa ajili ya mambo yake. 

Tausi amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia mtandao wa Facebook wa EATV na kusema kuwa yeye kwa mganga anakwenda wala hakuna tatizo 

"Nimewahi kwenda kwa mganga kwa ajili ya kazi za movie, kwetu ukitaka kuhama kwenda mkoa mwingine lazima utemewe mate, kwa hiyo nilikuwa nahama kuja Dar es Salaam nikaenda kwa mganga, lakini sijawahi kumroga mtu" alisema Tausi 

Mbali na hilo Tausi ameweka wazi kuwa mpenzi wake Prince Amigo hawezi kumuacha kwa kuwa kwake amekwama na hawezi kupinduka tena . 

Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA.