Jumamosi , 12th Oct , 2019

Rapa wa kike kutokea upande wa Kaskazini mwa Tanzania, yaani Arusha Dipper Rato, amefunguka kuhusu wanawake wa Arusha kuwa wakorofi, kutokuwa na mahaba na kutoa onyo kwa marapa wa kike Bongo.

Dipper Rato

Amesema hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kwa nini wanawake wengi wanaotokea mkoa wa Arusha, wanakuwa wakorofi kwenye mapenzi.

"Ukiwaingilia madem wa Chuga lazima ujipange na uangalie umeingia kwa mitikasi gani, stori zako ambazo unazileta kuanzia mwanzo ziwe hivyo hivyo usije ukaleta mapichapicha unabadilika na kutujazia mafaili lazima tukuzingue" amesema Dipper Rito.

Aidha ametoa onyo kwa wasanii wengine wa kike, ambao wanafanya muziki wa HipHop kama Rosa Ree, Chemical, Tammy The Baddest na wengineo.

"Kwa mimi hapa labda watu wajipange unajua mimi ni Dipper Rato, halafu kuhusiana na hizo issue za HipHop na Rege, Dance Hall nilikuwa wa kwanza kufanya mambo haya, mashabiki zangu na wafuatiliaji wa kazi zangu wanajua mimi ni nani" amesema Dipper Rato.