Jumatatu , 23rd Mar , 2015

Mpambano wa kuwania nafasi ya juu ya uongozi wa Jumuiya ya Hakimiliki ya kazi za wasanii nchini Kenya, MCSK umepamba moto baada ya msanii Lady B kupata ushindani katika nafasi hiyo, kutoka kwa staa wa muziki Frasha wa kundi la P-Unit.

msanii wa muziki wa injili nchini Kenya mwanadada Lady Bee

Kwa sasa wasanii hawa wote wanaendelea na kampeni zao kwa njia ya mtandao, Lady B akikazia suala la wanawake kupata muwakilishi kupitia nafasi hiyo kubwa, na Frasha akishikilia msimamo kuwa, jumuia hiyo inahitaji kiongozi anayeelewa vizuri mfumo wa muziki nchini Kenya unavyosonga.

Wasanii hawa kila mmoja kwa upande wake wameendelea kupata sapoti ya mastaa wenzao nyuma yao, huku uchaguzi wa chombo hicho muhimu kwa wasanii ukiwa umepangwa kufanyika mwezi ujao.