Jumamosi , 15th Feb , 2020

Msanii wa kike kutoka lebo ya "Free Nation" Nini amesema kilichobaki kwa sasa kati yake na Nay Wa Mitego ni mtu na boss wake na sio wapenzi kama ilivyokuwa  awali.

Picha ya Nini akiwa na Nay Wa Mitego

Msanii huyo amesema hayo kupitia show ya Friday Night Live "FNL" ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 9:00 hadi 5:00 usiku.

"Tulipokuwa tuna mahusiano kila mtu alijua na tulivyoachana tulisema, sasa hivi hatupo pamoja kwa muda mrefu sasa, nilimpost picha akinikumbatia kwa nyuma na nilichoandika kuhusu ile post  haijamaanisha kama ni mpenzi wangu na hatujarudiana, ila kama kuna ulazima wa watu kujua kama tupo kwenye mahusiano watajua tu" ameeleza Nini

Pia Nini ameendelea kusema  kwa sasa hivi yupo single na hataki kuwa kwenye mahusiano kwa sasa ila mwanaume anayemuhitaji anatakiwa awe mtanashati, mchapakazi na awe na hofu ya Mungu.

"Unajua kwenye mahusiano kuna mambo mengi unaweza ukampata mtu ambaye ni wa saizi yako lakini kuna vitu vingine mkashindwana, tulichoshindwana mimi na Nay Wa Mitego ni vitu ambavyo vimeshapita