Jumatano , 11th Sep , 2019

Wiki iliyopita ilitrend habari inayomhusu msanii Lulu Diva baada ya kuhojiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI na kusema kwa sasa ana umri wa miaka 19 na atarajiwa kuolewa akifikisha miaka 25.

Harmorapa na Lulu Diva

Leo limeibuka lingine katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa msanii Harmorapa ambaye ameandika kuwa amefikisha umri wa miaka 9 ikiwa ni miaka 10 pungufu ya Lulu Diva.

Harmorapa ameweka wazi kwamba ana umri huo baada ya kupost picha katika mtandao wa kijamii kisha kuandika,

"Namshukuru Mungu siku kama ya leo mwaka 2011 nilizaliwa kijana wenu Athumani Omary a.k.a supa staa Harmorapa, nawaomba muungane kunitakia kheri ya kusheherekea kwa kutimiza miaka 9 ya kuzaliwa".

Tulijaribu kumtafuta Harmorapa ili alitolee ufafanuzi kwa nini aliandika ana miaka 9 hali ya kuwa anaonekana mkubwa kuliko umri huo lakini hatukuweza kumpata.

Aidha rapa Nikki Wa Pili aliwahi kusema sababu za mastaa kudanganya umri zinatokana na kibiashara zaidi au mtu anaweza akakujaji kutokana na umri wako.

Usikose KIKAANGONI leo ambapo atakuwepo Amber Lulu. Kipindi kinaruka 'LIVE' katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Facebook na YouTube jina East Africa Television, ni kuanzia saa 8:30 hadi 9:30 mchana.