Ijumaa , 24th Jan , 2020

Mwanamuziki wa BongoFleva Lulu Diva, amesema anapenda sana kuvaa nguo fupi kwa sababu watu wakimuona waone maumbile yake yalivyopendeza, pamoja na michoro aliyoichora mwilini mwake.

Msanii Lulu

Lulu Diva ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuonekana amemuiga mchoro wa pajani, rapa wa kike nchini Marekani Cardi B.

"Wakati naichora hii Tattoo nilikuwa hata simjui huyo Cardi B mwenyewe, kwahiyo hata sijamuiga yeye nilikuwa na hili wazo tangu zamani, halafu mimi napenda sana kuvaa nguo fupi fupi sijui kwanini, kwahiyo nikivaa inatakiwa mtu alione paja lako limependeza nikaamua kuchora na tattoo ni urembo" amesema Lulu Diva.

Aidha Lulu Diva ameendelea kusema, mchoro wake huo aliouchora pajani sio mpya kwani una miaka mitatu, umefika hadi mgongoni.