Makundi mengine 5 yafuzu #2014Dance100

Jumamosi , 26th Jul , 2014

Usahili wa pili wa Dance 100% 2014 umekamilika kwa mafanikio makubwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay ambapo makundi 18 yameweza kujitokeza kushiriki.

Makundi yaliyofanikiwa kuingia hatua ya Robo Fainali leo Don Bosco Oysterbay wakitangazwa

Makundi haya ambayo yameonesha uwezo mkubwa kabisa mbele ya majaji Super Nyamwela, Lotus na Queen Darleen ni pamoja na The Mob, Inter Crew, The New Team, The Killer Makoba, Pambana Fasaha, The Warriors, Bustani, UB 40, Take Over Crew, Tatanisha Dancers, Wakali Sisi, Wakali Dancers, Wakali Dancehall, Wakushine, Fantastic Crew na Quality Boys.

Makundi yaliyofanikiwa kuingia katika ya robo fainali kutoka michuano hii ni pamoja na Wakali Sisi, Pambana Fasaha, Quality Boys, Bustani na Tatanisha Dancers.

Michuano hii imepambwa na burudani mbalimbali ikiwepo kundi la waendesha Baiskeli lililo chini ya Grand Malt ambao ni kinywaji rasmi cha mashindano haya kwa mwaka huu wakiwa sambamba na wadhamini Vodacom Tanzania, Kazi ni kwako.

Usaili mwingine utafanyika kwa mara ya mwisho mwishoni mwa wiki ijayo katika viwanja vya TCC Club Chang'ombe kutafuta makundi mengine matano yatakayoungana na idadi ya makundi 10 ambayo tayari yamekwishafuzu kuingia katika mashindano kwa sasa.