Man Fongo
Man Fongo amebainisha hayo baada ya kusakamwa takribani wiki moja sasa kwa kudaiwa kutumia kazi ya wasanii wenzake bila ya makubaliano ya aina yoyote waliyowekeana.
"Ni kweli nimepigiwa simu na watoto wa Baraka Mwishee wakitaka kufuatilia hati miliki ya ule muziki. Kwa hiyo hata kama kuna mtu mwingine anaona mimi nimemuibia muziki wake asiogope kufuatilia hati miliki kwa sababu huu muziki wetu tunausajili BASATA. So ukiwa unaongea ongea mimi najua ni 'blah blah' tu hizo wanaotafuta kiki kutoka kupitia mgongo wangu", alisema Man Fongo pindi alipohojiwa katika kipindi cha eNewz kutoka EATV.
Mtazame hapa chini Man Fongo akiendelea kufafanua baadhi ya vitu.





