Jumatatu , 26th Jul , 2021

Icon wa muziki wa Singeli Bongo Sholo Mwamba amesema Muna Love aache tabia ya kuchukua wavulana wadogo na kwenda kuishi nao kwani sifa hiyo inamuharibia kwenye kazi zake za utumishi wa Mungu.

Kulia ni Sholo Mwamba kushoto ni Muna Love

Sholo Mwamba anasema anafurahi kumuona Muna Love amebadilika katika nafasi yake ya Ulokole ila kitu ambacho anatakiwa akiache ni kuchukua vijana wadogo kwa sababu kinamuharibia CV yake.

"Muna mapenzi ni mama, namshukuru M/Mungu amebadilika katika nafasi ya Ulokole lakini sifa ambayo anatakiwa aiache maishani mwake ni kuchukua wavulana na kwenda kuishi nao, inamuharibia CV yake sisi wanaume tunahadithiana na stori nyingi nimezisikia kuhusu yeye" amesema Sholo Mwamba

Pia Sholo Mwamba amemshukuru Muna Love kwa kumpa sapoti kwenye muziki wake wakati anafanya kazi chini yake ya kumsimamia kwenye upande wa muziki.