Jumatatu , 21st Feb , 2022

Hitmaker ya ngoma ya bia tamu Marioo 'Toto Bad' anasema amehamia rasmi kuwa shabiki wa Klabu ya Yanga akitokea Klabu ya Simba.

Picha ya msanii Marioo

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari aliyofanya na Klabu Yanga Marioo anasema "Sasa nipo rasmi Yanga, zamani nilikuwa nashabikia ile timu nyingine. Mimi sipendi stress tuenjoy huu wimbo wa Yanga tamu".

Marioo alifahamika kama shabiki wa Simba na aliperform siku ya Simba Day katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ikumbukwe pia hata mkali wa muziki singeli Dulla Makabila alitangaza kuhamia Simba akitokea Yanga.