Jumapili , 19th Jul , 2015

Band ya dansi inayotikisa nchini Tanzania Mashujaa Music band wamepanga kuweka kambi mkoani Lindi kwa wiki mbili kujiandaa na album mpya baada ya kitikisa na album yao ya Risasi Kidole.

Rais wa Mashujaa Band kushoto Charles Baba akiwa na Meneja wa Band hiyo Martin Sospeter.

Akiongea na eNews meneja wa Mashujaa Martin Sospiter amesema lengo la kuweka kambi Lindi ni kuweza kuandaa nyimbo kwa utulivu na umakini wa hali ya juu ili kuwapa kilicho bora mashabiki wao.

Martini amesema mpaka sasa bado hawajaipa jina album yao inayokuja ila baadhi ya nyimbo tayari zimekwisha kamilika na zinachezwa katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni kama utangulizi wa Album hiyo.