Master J aeleza alichokatazwa na Baba yake

Alhamisi , 10th Oct , 2019

Producer mkongwe wa muziki wa BongoFleva Master J, ameshea jambo alilofundishwa kutoka kwa Baba yake Mzee Kimario, pamoja na 'issue' ya muonekano wa nywele zake alizokuwa nazo kwa muda mrefu.

Master J amesema hayo yote kupitia EATV & EA Radio Digital, mara baada ya kuulizwa kuhusu ukimya aliokuwa nao mpenzi wake Shaa, kwenye muziki ambapo amejibu.

Itabidi mumuulize yeye mwenyewe kwa sababu mimi kwenye upande wa muziki sihusiki kumsimamia na hiyo nilifundishwa na mzee wangu kwamba nisichanganye biashara na mambo ya familia “ amesema Master J.

Aidha kwa upande wa muonekano wa mavazi amesema, mpenzi wake Shaa huwa anampangia jinsi ya kuvaa na anapendelea avae mavazi ya suti ila yeye hapendi kutokana na hali ya hewa na binafsi anapendelea kuvaa Tshirt na Jeans.

Pia akiongelea kuhusu uwezekano wa kubadilisha style yake ya nywele, ambazo amezitunza kwa muda mrefu amesema

Zimenichukua muda sana, unajua vijana wa sasa hivi wanachukua nywele hizi wanaziunga ila mimi nimeanza nazo hizi zikiwa ndogo mpaka leo hii zipo hivi kwa hiyo nashindwa kuzikata, maana nimetoka nazo mbali ziadi ya miaka 7 na kubadilisha itakuwa sio rahisi” amesema Master J.