
Master J
Kuhusu 'issue' lawama anazopewa na baadhi ya wasanii kwa kuringa na kuwafukuza kipindi alichofanya nao kazi amesema,
"Zamani tulikuwa tupo makini na tunafanya muziki tofauti kidogo na vijana wa sasa hivi, kwanza nilikuwa na ratiba Jumatatu, Jumanne , Jumatano tunagonga 'beat' Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi ni siku ya kuingiza sauti kila mtu alikuwa na masaa mawili mawili"
Master J ameendelea kusema sasa hivi msanii anaanza na kunywa au mnapiga stori ila yeye kwake alikuwa bize kama atampangia tena msanii ratiba ni miezi mitatu, minne au sita ijayo kama akizingua alikuwa anawafukuza tu na ilikuwa kibiashara zaidi.
Pia amesema amefanya kazi na wasanii wengi sana ambao walikuwa wanazingua ila msanii pekee ambaye alikuwa hajawahi kusumbua ni A.Y