MC Pilipili amuonya mke wake

Jumanne , 14th Jan , 2020

MC Pilipili amesema hataki mke wake Qute Mena, awe msanii kwa sababu yeye tayari yupo katika tasnia hiyo, na asingependa afanye jambo hilo na badala yake ni kumtaka ajishughulishe na masuala mengine.

Picha ya MC Pilioili na mke wake Qute Mena

Akifunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, MC Pilipili amesema huwezi kumuoa mwanamke kwa taaluma yake bali unamuoa kwa unavyotaka wewe.

"Namheshimu mke wangu na nipo naye poa, sehemu kama hizi sipendagi kuja naye kwa sababu mimi ni msanii, mke wangu sio msanii na nisingependa kumleta kwenye sanaa, ningependa ashughulike anaweza kuwa Meneja wangu au Mkurugenzi lakini hawezi kuwa msanii, siwezi nikamleta sehemu za sanaa kwa sababu mimi naonekana" ameeleza MC Pilipili.

MC Pilipili ameendelea kusema "Hauwezi ukamuoa mwanamke kwa taaluma yake, unamuoa mwanamke kwa yeye mwenyewe unavyomtaka na kwa kuangalia kitu anachokifanya na anachokipenda ni hiki hapa, nisingependa mke msanii" ameongeza.