Mrembo wa Tanzania aibuka kidedea

Alhamisi , 6th Jun , 2019

Mrembo wa Tanzania Anitha Mlay, ameibuka kidedea katika mashindano ya Miss Landscape ya dunia yaliyofanyika nchini Australia

Anitha ambaye amefanikiwa kushika nafasi ya pili akitanguliwa na mrembo wa Marekani, ambaye ndiye aliyeshika nafasi ya kwanza, huku nafasi ya tatu ikienda kwa mrembo kutoka Colombia.

Shindano hilo la urembo la kimataifa linalobeba kampeni za utunzaji mazingira, kupiga vita ujangili pamoja na kutangaza utalii limeshirikisha warembo kutoka mataifa 41 huku Tanznaia ikiwa ni miongoni mwake.

Mratibu wa mashindano hayo nchini, Happy Maina amesema kwamba  ushindi wa Anitha ni wa taifa na pia ni jambo la kujivunia kwa kuweza kuiepeprusha bendera ya nchi vizuri.

Anitha ambaye anasoma stashahada ya sheria, amepeperusha vyema bendera ya Tanzania katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika jana, Juni 5, 2019.