Jumatano , 8th Jun , 2022

Msanii Msami Baby ameiambia PlanetBongo ya East Africa Radio kuhusu kupata msala wa kesi ya kuua mwezi wa pili mwaka huu ambayo ilimfanya kukaa ndani kwa wiki mbili.

Picha ya Msami Baby kwenye studio ya East Africa Radio

"Mwezi wa pili nilipata matatizo kidogo, nilishutumiwa kuua. Tulienda swimming jamaa mmoja akafariki ikaonekana labda sisi tumemuwekea madawa, kilichotusadia kulikuwa na CCTV Camera"

"Nilivyokamatawa nilikosa dili kubwa la Milioni 10, sikuwa na wasiwasi kwa kuwa hawakuwa na ukweli wa ile kesi, nilikaa wiki mbili kituo OysterBay" amesema Msami Baby 

Planet Bongo ya East Africa Radio ni kila siku ya J3 mpaka Ijumaa kuanzia saa 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.