Jumanne , 3rd Mar , 2015

Staa wa Muziki Noorah kutoka kundi la Chamber Squad, amepata pigo jingine kubwa baada ya kufiwa na mkewe kipenzi aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi.

Taratibu za msiba huo zinaendelea kupangwa huko Morogoro kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msanii Dark Master kama anavyoeleza zaidi hapa.

DARK MASTER

eNewz tunatoa pole na kumtakia faraja Noorah na familia yake na wote kwa ujumla ambao wanaguswa na msiba huo, na Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala Pema peponi aamin.