Alhamisi , 21st Jan , 2016

Rapa Country Boy, amesema kuwa kuongezeka kwa uwezo wake katika gemu, kujitambua na kuweza kuweka akiba ya kile anachokipata ni mabadiliko ambayo yamekuja katika maisha yakisababishwa na mwanaye Rakeem ambaye ana umri wa mwaka 1 sasa.

Rapa Country Boy wa nchini Tanzania

Rapa huyo mwenye umri mdogo na uwezo mkubwa kabisa, amesema kuwa mtoto huyo amekuwa ndio sababu ya yeye kufanya muziki sasa, hata mashabiki wakiona namna ambavyo uwezo wake umekuwa, lengo lake likiwa ni kumpa mtoto huyo maisha bora kuliko aliyoishi yeye.