Jumatano , 29th Sep , 2021

Mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma maarufu kama MwanaFA, amesema kwamba muziki si kipaumbele chake kwa sasa kwani kazi kubwa aliyonayo sasa ni kuwatumikia wananchi wake kwanza.

Mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma, maarufu kama MwanaFA

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 29, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, ambapo amesema kulingana na majukumu aliyonayo inafikia hatua anakosa hata muda wa kufanya mazoezi ili kuweka viungo vya mwili wake sawa.

"Suala la muziki kwa sasa kusema ukweli Mungu atusaidie tutaona namna itakavyokuwa kama tutaweza kufanya tutafanya, lakini ngoja tuwatumikie wananchi wa Muheza kwanza," amesema MwanaFA