Mwakyembe awaonya wasanii wa filamu kwenye hili

Jumamosi , 11th Jan , 2020

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amewataka wasanii wa filamu nchini kuzingatia suala la maadili kwenye filamu zao na yeyote atakayekiuka Serikali haitamvumilia.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe

Kauli hiyo ya Waziri Mwakyembe imewasilishwa na Kaimu wa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Kyando Kalonzo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tamthilia 2 ikiwemo ya Sarafu na Maisha Yangu ambao uliandasliwa naq Kampuni ya Multichoice Tanzania.

"Itumieni vizuri Bodi ya filamu, BASATA na COSOTA kwa kuwa hivi vipo kwa ajili yenu pia niwahase tuzingatia maadili yetu, pia Serikali itawachukulia hatua kali Wasanii wote ambao wanakiuka maadili" amesema Kyando Kalonzo kwa niaba ya Waziri Harrison Mwakyembe

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacqueline Woiso, amewataka Wasanii kushiriki kwenye tuzo Africa Magic Viewers Choice Awards ambazo zinaandaliwa na Kampuni hiyo.

"Tuna tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards naomba wasanii mjitokeze, 2019 tulikuwa na filamu zisizozidi 20."