Jumatatu , 28th Feb , 2022

Rapa asiyeishiwa na vituko Kodak Black kutoka nchini Marekani, ame-make headline mitandaoni baada ya kusema mwanaume haitaji kuwa anaoga kila siku bali kwa wanawake inafaa kuwa hivyo.

Picha ya msanii Kodak Black

Kodak Black amezungumzia hilo wakati wanazungumzia mada inayohusu masuala ya usafi ambapo anasema hata yeye sio mtu anayeoga kila siku, pia inawezekana mwanaume kutokuoga kila siku.

Pia ameongeza kusema anahisi wanaume na wanawake wana viwango tofauti linapokuja suala la usafi wa mwili.