Ijumaa , 19th Jan , 2018

Muongozaji wa Video  kutoka Kwetu Studio Director Msafiri, amejibu maswali yaliyokuwa yakiwasumbua watu wengi kuwa kama kuna ulazima kufanya video za Singeli kuwa za kinyamwezi.

Mkali huyo wa Video ameiambia Enewz kuwa Singeli itabaki kuwa 'Local' tu na kuufanya uwe wa Kinyamwezi ni kuupoteza muziki huo.

''Mziki wa Singeli unabidi kubaki kama ulivyo ili kudumisha tamaduni lakini pia kuupeleka kwa namna ambayo mziki huo unaitwa na kuchezwa na kuimbwa ili kuweza kuendelea kuuweka katika uasilia wake na kuzidi kuuufikisha mbali zaidi'', amesema Msafiri.

Pia Msafiri amesema ujumbe unaokuwa katika nyimbo hizo unabidi kufanyiwa video ambazo zitaendana na ujumbe wake kwa kuwa meseji ya mziki wa Singeli unafika haraka inaporekodiwa katika mazingira ambayo ni 'local' ili kuweza kuwatia moyo vijana wapambanaji.

Msafiri ameshauri kuwa pamoja na kwamba video za Singeli zinatakiwa kurekodiwa katika mazingira 'local' lakini haimaanishi kwamba kila nyimbo wadada wavae madera na suruali za kubana kisha kukatika viuno kwani hiyo sio staili pekee ya kucheza mziki huo.