"Nafanya mapenzi kila siku'' - TID

Jumatatu , 5th Aug , 2019

Msanii TID 'Top In Dar Es Salaam', amenyoosha maelezo juu ya suala zima la kufanya mapenzi na kutaka kumpa mbegu za uzazi msanii Lulu Diva.

TID amesema hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kwa wiki huwa anafanya mapenzi mara ngapi.

"Mimi kwa wiki naweza nisifanye kabisa mapenzi kwa sababu labda nakuwa nimechoka, kuwa na kazi nyingi au mpenzi wangu hayupo na siwezi kufanya mapenzi kama mwenza wangu hayupo ni hatari sana, ila kama mpenzi wangu yupo naweza kufanya nae kila siku kwa mwezi mzima inatokea tu".

Aidha msanii huyo amesema yupo tayari kupata watoto wowote ambao atakaojaliwa.

Pia ameeleza kuwa yupo tayari kutoa mbegu zake za uzazi kwa msanii wa kike Lulu Diva, ambaye hana mtoto ili aweze kupata watoto.

TID na Lulu Diva wamekuwa wakirushiana maneno kwenye vyombo vya habari baada ya TID kudai kuwa Lulu Diva ametelekeza mtoto.