"Nahitaji kijana anaevutia kama Usher" - Jide

Jumanne , 4th Mei , 2021

Komando na Dada Mkuu wa BongoFleva Lady Jaydee anahitaji kijana mwenye muonekano kama wa msanii wa RnB kutoka nchini Marekani Usher Raymond ili awepo kwenye video ya wimbo wake mpya.

Picha ya msanii Lady Jaydee na Usher Raymond

Lady Jaydee ameeleza kuvutiwa na mwanaume mwenye muonekano kama wa Usher Raymond pia ndio aina ya wanaume ambao anawapenda.

"Nakuja Arusha jamani, nikifika huko na-shoot video kabisa lakini nahitaji msaada wenu, nahitaji kijana anaevutia kama Usher ndio awepo kwenye video yangu maana wanaume wa hivyo ndio 'type' napenda, kwa hiyo hebu tisheni tuone watu wa Arusha" ameandika Lady Jaydee 

Kwa sasa Lady Jaydeea anajiandaa kufanya show yake mkoani Arusha ambayo itafanyika siku ya May 14.

Tazama interview ya Ibraah akimkana mrembo Nanah aliyemchora Tattoo