Jumatano , 30th Oct , 2019

Msanii wa BongoFleva nchini, Barakah The Prince, amesema kwa sasa ana maadui wengi sana ambao wanampangia mipango mibaya, ikiwemo kumkwamisha kwenye muziki wake na shughuli zake binafsi kwa namna moja au nyingine.

Barakah The Prince ameiambia EATV & EA Radio Digital, kuwa kuna watu tofauti tofauti na kwenye 'Angle" tofauti, ambao wanamkwamisha kufanya maendeleo yake na kutotaka afanikiwe.

"Mimi nina maadui wengi sana wengine wanaweza wakawa Dj's , mameneja , watangazaji wa Radio na Tv, kwa hiyo kuna watu tofauti tofauti na katika Angle tofauti, lakini unaweza ukawa na adui lakini siyo kwamba yeye ndiyo atakukwamisha, unaweza ukawa mtu unayecheka naye au kutembea naye ndiyo atakukwamisha" ameeleza Barakah The Prince.

"Pia nina maadui wengine ambao hata sijui kama ni maadui zangu, kuna watu wengine wanaweza wakawa wanakuchukia bila sababu wapo wanaochukuia maisha yako, kipaji chako, kazi yako na sio lazima awe adui yako au muwe maadaui na mtu yeyote ambaye anakuchukia hapendi ufanikiwe na akipata 'Target' ya kukukwamisha atakukwamisha tu" ameongeza.

Aidha Barakah The Prince amesema kuwa kauli zake hazijamlenga mtu yeyote, kwamba ndiye anamkwamisha katika kazi zake ila anajua wapo watu wanaopanga mipango mibaya kuhusu yeye