Jumatano , 19th Feb , 2014

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Nape Nnauye, leo hii amepata nafasi ya kuchat na umati mkubwa wa wapenzi wa ukurasa wa Facebook wa EATV na kuweka sawa madukuduku na maswali yao kibao kuhusiana na maisha yake binafsi pamoja na kisiasa.

eNewz imelifuatilia zoezi hili kwa karibu na pia kupata nafasi ya kuongea na Nape kuhusiana zoezi la Kikaangoni ambalo amelifurahia, lakini pia akatueleza kuhusiana na hobbie yake ya muziki pamoja na majukumu ya burudani anayosimamia katika chama chake ambapo ameeleza kuwa bendi zote za chama ikiwepo TOT zipo chini ya uongozi wake.

Mwanasiasa huyu mahiri pia amewataka watu kufahamu kuwa kila apatapo muda huwa anafanya mazoezi ya kupiga gitaa, na pia kwa sasa ameamua kurudi darasani kusoma zaidi muziki japokuwa amekiri kwa upande wa kuimba anaona kiwango chake kimeshuka kidogo.

Nape pia akatueleza kuhusiana na muziki wa kizazi kipya pamoja na kuweka wazi mapenzi yake kwa kazi za muziki za Mwana FA, Linah, Banana na Lady Jay Dee kati ya wengine ambao kazi zao kwa sasa anazihusudu sana.