Alhamisi , 2nd Jul , 2015

Navio, rapa kutoka Uganda ambaye kwa sasa ametoka na kolabo kali kabisa ya 'Ayaya' aliyoifanya na nyota Mr Blue wa hapa Tanzania, ameweka wazi kuwa rekodi hiyo ni zao la kuelewana na na kufanana sana kwa namna za ufanyaji kazi kati yao.

Wasanii wa muziki Navio wa Uganda na Mr Blue wa Tanzania

Navio ameeleza kuwa amekuwa akimfahamu Mr Blue kwa muda na katika wakati ambapo wamekuwa studio, kuzaliwa kwa rekodi kama 'Ayaya' kumepelekea kupata wazo la kufanya video ya kiwango na wazo rahisi, ambalo kwa kushirikiana na menejimenti limefanikiwa kuwa kazi ya mafanikio makubwa.