"Ndoa yangu nitaifanya kwenye meli" - Mkojani

Jumatatu , 12th Apr , 2021

Mchekeshaji maarufu kwa sasa nchini Tanzania Mkojani Mpango amesema anataka harusi yake iwe ya kitajiri na ataifanya baharini ndani ya meli ifikapo mwezi wa 7 mwaka huu.

Mchekeshaji Mkojani

Mkojani amesema ndoa yake ilipangwa kufanyika mwezi wa 3 mwaka huu lakini kutokana na mipango na sababu za kifamilia ikashindikana kufanyika, na lengo la kufanya harusi yake kwenye meli ni kutaka iwe na ukubwa wa aina yake.

"Nina mipango ya kuoa, ndoa yangu ilikuwa ifanyike mwezi wa 3 lakini sababu za kifamilia ikashindikana, harusi yangu nataka niifanye kwa ukubwa fulani iwe ndani ya meli na ya kitajiri, nadhani mwezi wa 6 au 7 itakuwa tumeshakamilisha hilo jambo, mchumba wangu tayari naishi nae na nimeshatoa barua" amesema Mkojani 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.