Jumamosi , 3rd Jun , 2017

Msemaji kutoka kundi la Weusi Nikki wa pili amejibu msanii Nyandu Tozi kwamba asitegemee majibu ya kashfa kutoka ndani ya kundi lao na kwamba kuzungumzia maisha yao binafsi kwenye vyombo vya habari siyo mipango yao bali muziki na masuala ya kijamii.

Nikki wa Pilli Kushoto, Kulia ni Nyandu

Nikki amejibu tuhuma hizo za Nyandu kupitia eNewz ya EATV kwa kusema kamwe Weusi hawawezi kuzungumzia maisha ya watu wengine pamoja na yao binafsi kwa sababu siyo malengo ya kundi lao na kuongeza kwamba maisha ya B.O.B hayawahusu hivyo hawawezi kuwaongelea .

"Nyandu ana uhuru wake wa kuzungumza lakini kamwe sisi hatutaweza kuzunguza yanayowahusu wao kwa sababu siyo kazi yetu. Tatizo 'mission' zao hazifanani na za kwetu, 'mission' za Weusi siyo za kuzungumza maisha yetu binafsi kwenye media au ya watu wengine kwa sababu hayatuhusu. Tutazungumza kuhusu muziki wetu,kazi zetu na muziki wetu" - Nikki wa Pili. 

Pamoja na hayo Nikki ametangaza hali ya hatari kwa ma rappa waliopo kwenye game juu ya ujio wake mpya unaotegemea kusikika siku chache zijazo  kwamba ubunifu, mashahiri pamoja na flow ni vitu ambavyo amejipanga kuwaaletea mashabiki zake.

Nikki amesema anawaonea huruma Mc's wengi kwani amekuja na mtindo tofauti wa mashahiri kitu ambacho kitazidi kumfanya aonekane bora katika game hii ya bongo.

Tazama hapa chini Nikki wa Pili alivyofunguka zaidi.