
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Nikki Mbishi anasema Prof. Jay amefanya kazi kubwa sana kumfanya yeye kuwa Nikki Mbishi kwani amekuwa akimtazama na kufuatilia kazi zake kwa muda mrefu na kusema yule ni mtu aliye mu inspire na anamkubali sana.
Mbali na Prof Jay Nikki Mbishi aliwataja wasanii wengine wanne ambao ni Hashimu Dogo, Fid Q, One Incredible pamoja na Stereo Singa Singa.