Ijumaa , 26th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu, amefunguka kuwa alishawahi kufuatwa kwa ajili ya kufanya video za utupu, lakini alikataa dili hilo.

Amber Lulu amesema kwamba kweli alifuatwa na kutakiwa kucheza video za utupu ili alipwe, lakini hakuweza kufanya hivyo kwani aliona kuwa atamkosea sana Mungu, ingawa changamoto zinazoshawishi watu kufanya vitu kama hivyo zipo nyingi.

Amber Lulu afunguka 

“Ilikuwa ni video ila nilikataa, 'sometimes' sisi ni binadamu, unakuwa umekunywa na au una stress, unaweza kujikuta unafanya kitu bila wewe kupenda, sasa kile kitu mtu anakuletea mezani utie sahihi, unakuta hatujapenda, lakini we do, ikitokea nimefanya ni sijapenda na sio kwa ridhaa yangu, usije ukafanya kitu uka'disapoint watu”, amesema Amber Lulu.

Amber Lulu ameendelea kwa kusema kwamba hata wanaofanya hivyo haamini kuwa wanafanya kwa uamuzi wao tu, bali huenda kuna hali inawasukuma kufanya hivyo.

Ikumbukwe kuwa Amber Lulu alijipatia umaarufu mkubwa kwa kupiga picha za nusu utupu, hadi zingine kumsababishia kuwa na kesi polisi baada ya kuvuja mitandaoni akiwa na msanii Young Dee, ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano.