"Niliumia kuachana na Amini, tunakuja" - Linnah

Jumatano , 10th Apr , 2019

Msanii wa Bongo Fleva, mwanadada Linnah amefunguka kuwa hakupenda kuachana na msanii Amini kwasababu alikuwa anampenda.

Linnah na Amini

Amesema hayo katika 'Interview' na Planet Bongo ya East Africa Radio, alipokuwa akitambulisha ngoma mpya aliyofanya pamoja na msanii huyo.

Alipoulizwa kuwa alijisikia vipi alipoachana na Amini, Linnah amesema, "kiukweli hakuna kitu kinauma kama kuachana na mtu unayempenda, mimi binafsi ninampenda Amini ndiyo maana niliumia".

"Hakuna asiyejua kuwa mimi na Amini tulikuwa wapenzi, kwahiyo watu wanaosema kuwa hivi sasa tumerudiana, hatuwezi kuwazuia kwa sababu wanapenda kutuona jinsi tulivyokuwa tukipendana", ameongeza.

Pia kuhusu uhusiano wa sasa baina ya wasanii hao ambao chimbuko lao ni THT, amesema kuwa atatafuta wakati rasmi wa kutambulisha penzi lao, lakini kwa sasa watambue tu kuwa wako pamoja na lolote linaweza kutokea.

Amini na Linnah kwa pamoja wametambulisha ngoma ya pamoja inayojulikana kama 'Nimenasa'.

Kumbukumbu ya penzi la Linnah na Amini

 

Taarifa za kurejea kwa penzi la wawili hao lilianza kusambaa hivi karibuni, ikiwa ni baada ya Amini kuachana na mkewe na Linnah kuachana na baba wa mtoto wake hivi karibuni. Wawili hao waliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi takribani miaka 8 nyuma, kiasi cha kutoa baadhi ya ngoma kadhaa pamoja.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.