Jumanne , 7th Jul , 2020

Muigizaji wa filamu na mchekeshaji Bongo Pili Kitimtim amesema mwanamke kujipiga kitaulo "kujichubua" ni lazima kwani hata yeye ameshajichubua vya kutosha, pia ameshea stori ya kukosa wanaume kutokana na kazi anayoifanya ya uchekeshaji.

Msanii wa filamu Pili Kitimtim

Akizungumzia kuhusu suala la kujichubua wakati anapiga stori na EATV & EA Radio Digital Pili Kitimtim ameeleza kuwa "Mimi sifeki maisha Nimejichubua vya kutosha mpaka hapa nilipo utakavyoniona Instagram ndiyo hapa nipo hivyohiyvo hakuna tofauti lazima nipige kitaulo mwanamke kung'aa, na haijawahi kuniletea madhara

Aidha Pili Kitimtim amesema kazi ya kuchekesha inamfanya kukosa wanaume ambao hudhani ni mcharuko kikukweli au dishi kuyumba kwa sababu anavyoigiza.

"Kitu ambacho kinanikosti kwenye maisha yangu ya uigizaji watu wananionaga mimi ni chizi kwa hiyo unaweza ukampenda mwanaume ukamfuata kumbe anakuona dishi limeyumba kwa hiyo tunakosaga wanaume tunavyocharuka kwenye TV" amesema Pili Kitimtim

Zaidi tazama kwenye video hapa chini