Msanii Barakah The Prince
Barakah The Prince amesema hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya Tundaman kumwambia alimsaidia nauli ya kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya ishu za kimuziki.
"Mimi sikuja Dar kwa bus nimekuja na ndege mtafute mama Bob Junior ndiye alikuja kunipokea Airport na gari lake, ila Tundaman alinisaidia kunipa Tour yake wakati anafanya show Mwanza, kipindi hicho ana wimbo wake na Spark na hakuna aliyekuwa hatamani kukutana naye" amesema Barakah The Prince
Mengine zaidi aliyoyazungumza Barakah The Prince kuhusu safari yake ya kufika Dar mtazame hapo chini kwenye video akieleza zaidi.




