'Nimeshafumaniwa zaidi ya mara 75' - Miss Bella

Ijumaa , 10th Jan , 2020

Mrembo ambaye ni msanii wa filamu na muziki, Miss Bella, amesema tangu amezaliwa kwenye mahusiano yake ameshafumaniwa zaidi ya mara 75, na mwanaume akiwa kwake hawezi kumuacha mpaka yeye atakapoamua.

Picha ya Miss Bella

 

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Miss Bella amesema ni kweli ameshafumaniwa mara zote hizo na kwa siku huwa anatongozwa na wanaume 50 hadi 150.

"Mimi nimeshafumaniwa zaidi ya mara 75 tangu nizaliwe, mimi ni Mmakonde mwanaume akiwa kwangu habanduki mpaka niamue mwenyewe  na nimeshapiga sana tu, na kwa siku natongozwa na wanaume 50 hadi 150 kwenye ujumbe wa mtandao wa Instagram, lakini huwa nachagua wa kuwa naye" ameeleza Miss Bella. 

Aidha Miss Bella ameendelea kusema "Kuna muda huwa unavunja mahusiano na mtu wako, na wewe unataka kufanya mapenzi hivyo lazima utafute mtu wa kufanya naye, halafu mimi bado ni binti, msichana kabisa hata miaka 32 sijafika kwahiyo mapenzi ni lazima".

Miss Bella aliwahi kutangaza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwana Hiphop Godzilla, ambapo watu walidai kama anatafuta kiki.